Bus Online Booking Service

Bus Online Booking Service! / Huduma ya Kufanya Booking za Mabasi kwa Mtandao!

Bus Online Booking Service is a service of Kicheko Ltd of Moshi, a well established ICT Service Provider since 2001. Kicheko Ltd has a range of technology related services including Internet Service Provider, Computer Service and Maintenance, ReaDisc virtual library service, Internet Cafe, Web to SMS service and Bus Online Booking Service. / Huduma ya Kufanya Booking za Mabasi kwa Mtandao ni huduma inayotolewa na kampuni ya Kicheko Ltd ya Moshi, ambayo ni kampuni maarufu kwa kutoa huduma za mtandao toka mwaka 2001. Kampuni ya Kicheko Ltd ina huduma kadhaa katika nyanja ya teknolojia ya habari na mawasiliano kama vile huduma ya kuunganisha internet (ISP), huduma ya kuuza, kufanya service na matengenezo ya kompyuta, huduma ya Maktaba Pepe inayoitwa "ReaDisc", huduma ya Internet Cafe, huduma ya kutuma SMS nyingi kwa mara moja kwa kutumia kompyuta na huduma ya kufanya booking ya safari za mabasi kwa mtandao.

Bus Online Booking Service іѕ an online service for booking a bus trip and pay online well before the date of travel. This is a pre-booking and pre-paid service with a time cut-off of 30 hours before the time of travel which means it is not available one day before date of travel and on the date of travel. For those days you have to book manually at the Bus Operators booking office. / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao ni huduma inayokuwezesha kufanya booking ya safari ya basi, kukata tiketi na kuilipia kabla ya siku ya safari. Hii ni huduma ya kufanya booking kabla ya siku ya safari na kulipia kabla ya siku ya safari. Huduma hii inapatikana hadi masaa 30 kabla ya safari yaani unaweza kufanya booking mapema lakini siku moja kabla ya safari na siku ya safari huduma hii haifanyi kazi na badala yake kwa siku hizo ni lazima ufanye booking kupitia ofisi za booking za basi husika.

Bus Online Booking Service is a "booking" service and does not provide bus services. This service facilitates booking and ticket purchase and therefore its obligation starts from the moment you make your booking and ends the moment you have been allowed to board the bus and take your pre-booked seat. From that moment the responsibility for your travel shifts to the Bus Operator company who has the responsibility to make sure you travel safely and comfortably to your destination. / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao ni huduma ya kukuwezesha kufanya "booking" na siyo kutoa huduma ya usafiri. Huduma hii inawezesha kufanya booking na kununua tiketi na kwahiyo wajibu wake unaanzia pale unapofanya booking na kuishia pale unapokubaliwa kuingia katika basi na kukaa katika kiti chako tayari kwa safari. Kuanzia wakati huo wajibu unahamia kwa kampuni ya basi husika ambayo itawajibika kuhakikisha unasafiri kwa raha na salama hadi mwisho wa safari yako.

The aim of Bus Online Booking Service іѕ tо gіvе the bеѕt service to оur various clients securely, reliably and аt аffоrаblе рrісе. It takes away the guess work and trouble of traveling all the way to the bus booking office without knowing whether there is a scheduled bus or not, whether seats are available or not, and intriduce transparency in terms of bus schedules, timetable, fares, etc. The customer saves time, pay the legally approved fare, and escape the bother of tauts and ticket raketeers.  / Madhumuni ya huduma ya kufanya booking za mabasi kwa njia ya mtandao ni kurahisisha utaratibu mzima wa kufanya booking za mabasi kwa kuweka wazi ratiba za mabasi, nauli, upatikanaji wa nafasi, na pia kuokoa muda wa kusafiri hadi ofisi za kufanyia booking bila kujua kama basi lipo au halipo, nafasi ipo au haipo, na bila uhakika wa nauli itakayotozwa. Hii pia inaepusha adha ya wapiga debe na walanguzi wa tiketi na vibaka.

At Bus Online Booking Service, we аrе inceasingly progressing by making research continuously аnd improving оur ѕеrvісеѕ to thе hіghеѕt ѕtаndаrdѕ taking into consideration our situation and priorities of our customers. Our сlіеnt'ѕ іntеrеѕt is оur priority especially in overcoming unneccessary hurdles and bureaucracy. Wе are mіndful оf building a hеаlthу rеlаtіоnѕhір with оur сuѕtоmеrѕ, bus operators, sub-contractors аnd соnѕultаntѕ. Our gоаl іѕ to foster co-operation and tеаmwоrk at all levels tо achieving a grand ѕuссеѕѕful рrоjесt. / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa njia ya mtandao inaendelea kujiboresha  kila uchao kwa kufanya tafiti mbalimbali ili kuongeza viwango vya ubora wa huduma hii kwa kuzingatia mazingira halisi ya nchi yetu na vipaumbele vya wateja wetu. Tunathamini sana maslahi ya wateja wetu hasa katika kuwaondolea adha na usumbufu usio na sababu. Tunapenda sana kujenga uhusiano imara na wateja wetu ikiwa ni pamoja na kampuni za mabasi.

Please note that Bus Online Booking Service has a cut-off booking time of 30 hours before travel date and time. That means you can only do your booking online by using Bus Online Booking Service up to two days before date and time of travel. The last day before travel and the day of travel all bookings are done manually at the Bus Operator's booking offices as they are being done in the past. This is done deliberately to avoid conflicts of last minute double booking online and manually. / Tafadhali zingatia kuwa huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao ni huduma inayopatina hadi masaa 30 kabla ya siku na saa ya safari. Hiyo ina maana unaweza kutumia huduma hii hadi siku mbili kabla ya safari. Siku moja kabla ya safari na siku ya safari huduma hii haitapatikana na badala yake wateja watatakiwa kufanya booking katika ofisi za mabasi kama ilivyokuwa hapo zamani. Hii imefanyika kwa makusudi ili kuondoa uwezekano wa mkanganyiko wa kufanya booking mara mbili katika dakika za mwisho.

Bus Online Booking Service recognise the buyer of the ticket as being a separate person from the passenger who travels. It could be same person in which case same information will be entered on both fields. / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao inamtambua "Mnunuzi" wa tiketi kuwa mtu tofauti na "Abiria" atakayesafiri. Kwa sababu hiyo wakati wa kufanya booking utatakiwa kuingiza taarifa za wote wawili na endapo ni mtu huyo huyo basi taarifa hiyo hiyo itarudiwa kwa kujazwa sehemu zote mbili za Mnunuzi na Abiria.

For frequent travelling customers who would like their details to remain in the system and avoid typing them in everytime they want to make a purchase, they can register by following the Registration link under Agents sub-menu. They will get an email to confirm and activate their account. Next time they just login using the Login link under Agents sub-menu and their details will be picked up immediately and filled in the ticket purchase buyer form. / Kwa wateja wanaosafiri mara kwa mara ambao wangependa taarifa zao zibaki kwenye system na kutolazimika kuziingiza kila wanapotaka kukata tiketi, wanaweza kujisajili kwa kufuata menyu ya "Registration" chini ya Booking Agents. Utatumiwa barua pepe kuthibitisha na kila wanapotaka kufanya booking wataingia kwenye system kwa kutumia menyu ya "Login" hapo hapo chini ya Booking Agents..

Bus Online Booking Service takes your feedback and comments seriously. If you have something to say which will help us improve our service please do not hesitate to contact us by using the "Contact" page. If your comment is long then email us at This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it. / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao inathamini sana mrejesho na maoni yako hususan kwa wewe ambaye umeshawahi kutumia huduma hii. Tutashukuru sana kusikia toka kwako kama una jambo lolote ambalo unadhani litaweza kutusaidia kuboresha zaidi huduma hii. Wasiliana nasi kwa kutumia menyu ya "Contact" au kama ni maelezo marefu tuandikie barua pepe kwa anuani ya This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it..

You are most welcome! / Karibu sana!

© Copyright 2017 Kicheko Ltd, All rights reserved