Fast Safe Reliable

Fast, Safe and Reliable Service! / Huduma ya Haraka, Salama na ya Uhakika!

Bus Online Booking Service is a very fast, safe and reliable service. Some of the advantages of booking online by using Bus Online Booking Service are: / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao ni ya haraka, salama na ya uhakika. Baadhi ya faida za kufanya booking kwa mtandao ni pamoja na:

1. You can now book your trip from the comfort of your sofa at home or your desk at home or office, while travelling in the country or abroad, anytime of the day or night, as long as you have internet on your mobile phone, tablet, ipad, laptop or desktop computer, or Internet Cafe, you can do your booking and purchase your ticket online and in real time. The whole procedure takes less than 15 minutes. It is that fast and easy! / Sasa unaweza kufanya booking ya safari yako ya basi ukiwa nyumbani, kazini au hata safarini nchini au nje ya nchi, wakati wowote asubuhi, mchana, jioni au usiku kwa kutumia simu yako ya mkononi, ipad, tablet, laptop au kompyuta ya mezani, au Internet Cafe, unaweza kufanya booking na kununua tiketi kwa ajili ya safari yako na kuchapisha tiketi ya safari hapo hapo ulipo wakati huo huo. Utaratibu mzima unachukua chini ya dakika 15. Ni haraka na rahisi kabisa. 

2. The fact that you do not have to wait till working hours for the booking office to open and you do not have to travel all the way to the booking office without even knowing whether there are buses available and which seats are not booked yet, this service puts you in command of the booking process since you can book anytime, from anywhere, with full knowledge of available buses, available seats, prices and that allows you to choose a bus of your choice, choose a convenient time to start your journey and your preferred seat. / Ukweli kuwa huhitaji kusubiri had saa za kazi ili ofisi ya kufanya booking ifunguliwe na huhitaji kusafiri hadi ilipo ofisi ya kufanya booking bila kujua kama kuna basi, kama kuna nafasi, bei ya tiketi, huduma hii inakupa mamlaka ya kutawala mchakato mzima wa kufanya booking yako kwa sababu unaweza kufanya booking wakati wowote, mahali popote, ukiwa na taarifa zote za mabasi yaliyopo, viti vilivyo wazi, bei za tiketi na hivyo kukuwezesha kuchagua basi unalotaka, muda wa kuanza safari na kiti unachopenda.

3. The option to book a return journey add more assurance that you will actually get a bus to take you back home at the end of your current trip. Since everything is documented you are assured of being able to travel back even in those days of hectic travel when the schools are closing or during festive season. We are still talking to bus operators to consider a discount on a return ticket in order to encourage travellers and cultivate loyalty. / Uwezekano wa kufanya booking ya safari ya kurudi inakuongezea uhakika kuwa hutakosa usafiri wa kurudi hata nyakati ambapo unafiri unakuwa wa shida kama nyakati za sikukuu za mwisho wa mwaka na wakati shule zinapofungwa. Bado tunaongea na kampuni za mabasi na tunaamini kuwa wataona mantiki ya kutoa punguzo kwa safari ya kurudi kama mtu atafanya booking wakati mmoja na safari ya kwenda ili kuwahamasisha watu kusafiri na kujenga utiifu.

4. The booking process is very safe since all online transactions are monitored and recorded. Once you pay for your ticket notification emails are sent to the person who bought the ticket, the person who will travel, to Bus Online Booking Service, and to the Bus Operator whose bus you have booked. On the day of travel you just need an ID together with your ticket number to be allowed to board the bus since all ticket details will already be recorded on the system and can be retieved if so needed. / Mchakato mzima wa kufanya booking kwa mtandao ni salama kwa sababu miamala yote kwenye mtandao ina kumbukumbu na inafuatiliwa kwa makini. Ukishalipia tiketi yako taarifa inapelekwa kwako uliyelipa, kwake atakayesafiri, kwa mwenye kutoa huduma ya kufanya booking ya mabasi kwa mtandao, na kwa kampuni ya mabasi utakayosafiri nayo. Siku ya safari unahitaji Kitambulisho na namba ya tiketi ili kuruhusiwa kuingia ndani ya basi kwa sababu taarifa zako zote tayari zitakuwa zimerekodiwa ndani ya system na zinaweza kuchapishwa pindi zitakapohitajika.

5. This service of online booking is much safe for the traveller since you do not have to wriggle your way through hosts of tauts some of whom are not very sincere and hike ticket prices especially when demand is high. There are also cases of complaints by passengers being mishandled by tauts. By booking online you avoid all those hussles as your ticket is already paid and your seat reserved. / Hii huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao ni salama zaidi kwa msafiri kwa sababu inakuepusha na bugudha ya wapiga debe ambao baadhi yao si waaminifu na wengine ni walanguzi wa tiketi has wakati mahitaji yanapokuwa makubwa. Kuna visa vya abiria kudhulumiwa na hata kuibiwa na wapiga debe. Kwa kutumia huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao unaepuka adha zote hizo kwani tiketi yako inakuwa tayari imeshalipiwa na kiti chako kimehifadhiwa.

6. The online booking service is also good for Bus Operators since they get true and actual revenue from the tickets which had been sold. Manual booking is prone of mischievous activities including under declaration of revenue and outright theft. Both the Bus Operators and the revenue collection agencies will now have a reliable platform to read actual revenue and account for it accordingly. / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao pia ina manufaa kwa kampuni za mabasi kwa sababu watapata mapato yao ya ukweli na halisi kutokana na mauzo ya tiketi. Utaratibu wa zamani wa kufanya booking kwa mkono ofisini unachelewesha kupata taarifa za mauzo na ni rahisi kuhujumiwa kwa sababu unahusisha watu wengi katika hatua na ngazi tofauti. Kampuni za mabasi na Mamlaka ya Mapato kwa kutumia mfumo huu wa kufanya booking za mabasi kwa mtandao wataweza kupata taarifa sahihi za mapato katika muda muafaka na kuwajibika ipasavyo.

7. The Bus Online Booking Service generate a passenger manifest for each trip which is important both for the bus company to know and track its loyal customers and for safety agencies like SUMATRA and the Police Force to track identities of passengers in the unlikely event of an accident. / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao inatengeneza orodha ya wasafiri katika kila basi kwa kila safari ambayo ni muhimu kwa kampuni ya mabasi kujua wasafiri wake na hata mamlaka za usalama wa safari kama SUMATRA na Jeshi la Polisi wanaweza kupata taarifa sahihi za watu waliosafiri endapo patatokea ajali au shida nyingine.

8. The Bus Online Booking Service is very reliable after being used extensively in online airline booking and being ported for bus operations. There are many years of research and development as well as practical usage experience which attest to its proven reliability. / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao ni ya uhakika baada ya kutumika kwa muda mrefu katika booking za usafiri wa anga na kuundwa upya kwa ajili ya usafiri wa mabasi. Kuna miaka mingi ya utafiti na maendeleo pamoja na uzoefu unaotokana na matumizi halisi ambavyo vyote vimechangia ubora na uthabiti wake usio na shaka.

© Copyright 2017 Kicheko Ltd, All rights reserved