Terms and Conditions

Terms and Conditions / Vigezo na Masharti

This Terms of Service is a legal agreement between you and Kicheko Ltd that governs your access to and use of the Bus Online Booking Service as a purchaser of booking service and bus ticket. Please review this entire Terms of Service before you decide whether to accept it and continue with the booking process. / Vigezo na Masharti haya ni mkataba wa kisheria kati ya kampuni ya Kicheko Ltd, ambayo ndiyo inamiliki na kuratibu mfumo huu wa kufanya booking za mabasi kwa mtandao, na wewe ambaye ndiye mtumiaji wa mfumo huu na mnunuzi wa tiketi. Tafadhali soma kwa makini vigezo na masharti haya kabla ya kuamua kukubali na kuendelea kufanya booking.

Definitions / Tafasiri

The following defined terms appear in this Terms of Service: / Tafasiri ya maneno yaliyotumika katika vigezo na masharti haya:

   Bus Online Booking Service: A "service" of booking and buying a ticket online, provided by Kicheko Ltd. / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao: Ni "huduma" ya kufanya booking na kununua tiketi kwa mtandao, inayotolewa na kampuni ya Kicheko Ltd. 

   Bus Operator: The company which owns the buses and provide bus travel service. / Kampuni ya mabasi: Ni kampuni inayomiliki mabasi na kutoa huduma ya kusafirisha abiria toka sehemu moja hadi nyingine. 

   Buyer: The person who purchase a ticket for Travel Service. Might be same or different from the Passenger. / Mnunuzi: Mtu anayenunua tiketi kwa ajili ya safari. Anaweza kuwa mtu tofauti na abiria atakayesafiri. 

   Customer: A person who registers and use the Bus Online Booking Service as a Buyer or Passenger. / Mteja: Mtu anayejisajili na kutumia huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao kama Mununuzi au Abiria.

   Passenger: The person who consumes the travel service by travelling. / Abiria: Mtu anayetumia huduma ya usafiri kwa kusafiri.

  Payment Instrument: The mobile payment option that is registered by a Customer with the Service or credit card or debit card to facilitate the processing of online Payment Transactions. / Chombo cha Malipo: Ni namna mojawapo ya kufanya malipo iliyosajiliwa na Mteja ikiwa ni pamoja na malipo kwa njia ya simu au njia ya kadi ili kuwezesha malipo kwa njia ya mtandao.

   Payment Service Provider: The financial institution which holds Buyer's money and transfer the funds during processing of a payment through the Bus Online Booking Service. / Huduma ya Malipo: Huduma ya kununua au kutuma fedha kwa mtandao kupitia kadi za benki kama Visa na Mastercard na pia kupitia kampuni za simu kama Mpesa na Tigopesa.

  Payment Transaction: The processing of a payment through the Bus Online Booking Service that results in the debiting or charging of the Purchase Amount to a Buyer’s Payment Instrument and the crediting of funds to a Seller. / Muamala: Machakato wa kufanya malipo kupitia huduma ya booking za mabasi kwa mtandao ambao unaishia kwa kutoa fedha za manunuzi ya tiketi kutoka katika Chombo cha Malipo cha Mnunuzi na kuzipeleka fedha hizo kwa Muunzaji.

    Product: Travel service that is listed for sale by Bus Operator that a Buyer may pay for by using the Bus Online Booking Service. / Bidhaa: Huduma ya usafiri iliyotangazwa kuuzwa na Kampuni ya Mabasi na ambayo Mnunuzi anaweza kuinunua na kuilipia kwa kutumia huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao.

    Purchase Amount: The amount of a Payment Transaction to pay for the Product, and any related fees, taxes or charges, as applicable. / Kiasi cha Malipo: Kiasi cha muamala kinacholipiwa bidhaa, pamoja na ada, kodi, au gharama, kama zinahusika.

   Seller: The Bus Operator who sales the Travel Service to the Buyer. / Muuzaji: Kampuni ya mabasi inayouza huduma ya usafiri kwa Mnunuzi.

Service: The Bus Online Booking Service, described in this Terms of Service, that facilitates the processing of a booking and online payment transactions to buy a bus ticket on behalf of a Seller. / Huduma: Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa njia ya mtandao, ambayo imefafanuliwa katika vigezo na masharti haya, kwamba inawezesha kufanya booking na kulipia tiketi kwa mtandao kwa niaba ya Muuzaji.

   “We”, or “us”: Kicheko Ltd who is the company providing the Bus Online Booking Service. / "Sisi": Kampuni ya Kicheko Ltd ambayo ni kampuni inayotoa huduma ya kufanya booking za mabasi kwa njia ya mtandao.

   "You": A Customer that registers to use, or uses, the Bus Online Booking Service to make travel booking and online payment transactions to buy a ticket. / "Wewe": Mteja uliyesajili kutumia, au unayetumia, huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao, kufanya booking ya safari na kufanya malipo kwa mtandao ili kununua tiketi.

Requirements for Registration / Mahitaji ya Usajili

In order to use the Bus Online Booking Service, you hereby consent to provide and agree to complete all required information elements on the Service registration web pages. You must register a valid mobile payment option as a Payment Instrument or use a Credit or Debit Card to make Payment Transactions and pay fees and other obligations arising from your use of the Service. You undertake and agree to provide current, complete and accurate information and maintain it as current and accurate. We may require you to provide additional information as a condition of continued use of the Service, or to assist in determining whether to permit you to continue to use the Service. / Ili kutumia huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao, unaridhia kutoa taarifa zote zinazohitajika na kujaza fomu zote utakazohitajika kujaza katika tovuti ya kujisajili na huduma. Ni lazima usajili chombo cha malipo kilicho sahihi kwa ajili ya kufanya miamala na kulipa ada ya huduma na mahitaji mengine yanayohusiana na kutumia huduma kama yapo. Unaahidi na kukubali kutoa taarifa zilizo sahihi, zilizokamilika, na zilizo sahihi. Tunaweza kukuhitaji kutoa taarifa zaidi au uthibitisho ili uweze kuendelea kutumia huduma hii, au kukutaka utusaidie kufanya uamuzi kama tukuruhusu uendelee kutumia huduma hii.

We, in our sole and absolute discretion, may refuse to approve or may terminate existing registrations with or without cause or notice, other than any notice required by any applicable law, and not waived herein. / Sisi, kwa utashi wetu wenyewe, tunaweza kukataa kuridhia usajili au kusimamisha usajili uliokwisha fanyika kwa sababu yoyote ile au hata bila sababu yoyote, bila kuwajibika kutoa taarifa yoyote, isipokuwa taarifa itakayohitajika kisheria, na ambayo haikuondolewa hapa.

By agreeing to this Terms of Service for Buyer, you represent that you are: / Kwa kukubali vigezo na masharti haya kwa Mnunuzi, unathibitisha kuwa:
    18 years old or older; and / Una umri wa miaka 18 au zaidi; na
    capable of entering into a legally binding agreement. / Una uwezo wa kuingia mkataba wa kisheria.

Payment Transaction Processing / Mchakato wa Malipo

    You acknowledge and agree that your processing of a booking and purchase of tickets are transactions between you and the Bus Company, and not with Bus Online Booking Service. Bus Online Booking Service is not a party to Buyer’s purchase of travel service, and Bus Online Booking Service is not a buyer or a seller in connection with any Payment Transaction, unless expressly designated as such in the listing of the product on a Bus Online Booking Service website. / Unathibitisha na kukubali kuwa kufanya kwako booking na kununua tiketi kwa mtandao ni biashara kati yako na Kampuni ya mabasi, na siyo kati yako na huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao. Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao siyo sehemu ya Mnunuzi anayenunua huduma ya usafiri, na pia siyo Muuzaji wa Mnunuzi katika mchakato wa malipo isipokuwa pale ilipoainishwa hivyo katika tovuti ya huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao.

    The Bus Online Booking Service is a facilitation service which facilitates the processing of a travel booking and Payment Transactions to complete a payment for a purchase of ticket between a Buyer and a Seller. The Service will store information from Buyers, such as their Payment Instruments, and will process Payment Transactions on behalf of Sellers through the Payment Service Provider. The payment service provider may delay payment processing of suspicious transactions or transactions which may involve fraud, misconduct, or violate applicable law, this Terms of Service for Buyers, or other applicable Bus Online Booking Service policies, as determined in Bus Online Booking Service’s sole and absolute discretion. Buyer authorizes the charge or debit to Buyer’s Payment Instrument as necessary to complete processing of a Payment Transaction. Buyer also authorizes the crediting to Buyer’s Credit in connection with reversals, refunds, or adjustments through the Service. / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao ni huduma ya uwezeshaji ambayo inawezesha kufanya booking na kununua tiketi kwa mtanado kati ya Muuzaji na Mnunuzi. Huduma hii itahifadhi taarifa kutoka kwa Wanunuzi, kama vile chombo cha malipo, na kufanya malipo kwa niaba ya Muuzaji kupitia Huduma ya Malipo. Huduma ya Malipo inaweza kuchelewesha kukamilisha mchakato wa malipo iwapo kama kuna viashiria vya kughushi, uhalifu, uvunjwaji wa sheria, ukiukwaji wa vigezo na masharti haya kwa Mnunuzi, au ukiukwaji wa sera nyingine yoyote ya huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao. Mnunuzi anatoa idhini kwa chombo chake cha malipo kutoa fedha na kuzituma kwa Muuzaji ili kukamilisha muamala. Mnunuzi pia anatoa idhini ya kuingiza fedha katika chombo chake cha malipo kama kutakuwa marejesho au marekebisho.

    You acknowledge and agree that payments to requests from other Buyers are transactions between you and the Buyer and not with Bus Online Booking Service. / Unathibitisha na kukubali kuwa malipo kwa mujibu wa maombi ya Wanunuzi wengine ni biashara kati yako na hao Wanunuzi na siyo kati yako na huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao.

    You acknowledge and agree that you are not able to withdraw money from the Bus Online Booking Service and payment transaction. / Unathibitisha na kukubali kuwa hutaweza kutoa fedha kutoka kwenye huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao baada ya muamala kukamilika.

Limitations on the Use of Service / Mipaka ya Matumizi ya Huduma

    We reserve the right to change, suspend or discontinue any aspect of the Bus Online Booking Service at any time, including hours of operation or availability of the Service or any Service feature, without notice and without liability. We also reserve the right to impose limits on certain Service features or restrict access to parts or all of the Service without notice and without liability. 
We do not warrant that the functions contained in the Service will be uninterrupted or error free, and we shall not be responsible for any service interruptions (including, but not limited to, power outages, system failures or other interruptions that may affect the receipt, processing, acceptance, completion or settlement of Payment Transactions or the Service). / Tunahifadhi haki za kubadili, kusimamisha au kuondoa sehemu yoyote ya huduma ya kufanya booking kwa mtandao wakati wowote, ikiwa ni pamoja na masaa ya kufanya kazi, au muda wa kupatikana kwa huduma, au sehemu yoyote ya huduma, bila kutoa tarifa wala kuwajibika. Tunahifadhi pia haki za kuweka mipaka ya matumizi ya huduma au kuzuia kutumika sehemu au huduma nzima bila kutoa taarifa wala kuwajibika. Hatutoi dhamana kuwa mfumo unaoendesha huduma hii hautakuwa na makosa wala hakutakuwa na nyakati utashindwa kufanya kazi na hatutawajibika kwa matatizo yoyote yanayoweza kupelekea huduma kutopatikana (ikiwa ni pamoja na kukatika umeme, kuharibika mitambo, au matatizo mengine yanayoweza kuathiri kupokea, kuchakata, kukamilisha miamala au huduma).

    We may limit or suspend your use of the Bus Online Booking Service at any time, in our sole and absolute discretion. If we suspend your use of the Service, we will attempt to notify you by electronic mail and/or SMS. / Tunaweza kukuwekea mipaka au kusimamisha matumizi yako ya huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao wakati wowote, na kwa uamuzi wetu wenyewe. Kama tukisimamisha matumizi yako ya huduma tutakufahamisha kwa email au ujumbe mfupi kupitia simu ya mkononi.

Privacy / Faragha

You understand and agree that personal information provided to us in connection with the Bus Online Booking Service is subject to the Service’s Privacy Policy. / Unaelewa na kukubali kuwa taarifa binafsi tulizopokea katika matumizi ya huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao zitafanyiwa kazi kwa mujibu wa Sera ya Faragha ya huduma hii.

Service Fees / Ada ya Huduma

We charge a fee to the Person doing the booking or buying the Ticket as a Buyer. We do not charge our service fee to the Seller who are the Bus Operating Companies. Service fee include cost of all applicable associated services provided, such as online payment processing through the Payment Gateway, SMS, Email, maintenance and costs associated with the whole communication system. We do not charge or cover fees associated with your Payment Service Provider like credit or debit card fees, and mobile money  fees. / Tunatoza ada ndogo kwa mtu anayefanya booking au kununua tiketi kama Mnunuzi. Hatutozi ada ya huduma kwa Muuzaji wa huduma ya usafiri ambayo ni kampuni ya mabasi. Ada ya huduma inajumuisha gharama ya huduma zote zinazohusika na mchakato huo kama gharama za kufanya malipo kwa mtandao, gharama za kutuma ujumbe wa SMS, gharama za email, gharama za kusimamia na kuendesha mfumo mzima wa mawasiliano. Hatutozi wala kujumuisha gharama za Huduma za Malipo kupitia chombo chako cha malipo kama kutuma fedha kwa mitandao ya simu au kadi za benki.

Disputes / Mizozo

Bus Online Booking Service will provide various tools to assist Customers in communicating with each other to resolve a dispute that may arise between Buyers and Sellers with respect to their transaction. If Customers are unable to resolve a dispute, we can mediate disputes between buyers and sellers if either party requests assistance. / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao itatoa nyenzo na taarifa mbalimbali kusaidia Wateja kuwasiliana na kutatua mzozo unaoweza kutokea kati ya Muuzaji na Mnunuzi katika kutumia huduma hii. Kama Wateja hawataweza kutatua mzozo kati yao, tunaweza kuwa wasuluhishi kati ya Muuzaji na Mnunuzi kama upande wowote utahitaji msaada wetu.

Termination of Service / Kusitisha Huduma

We reserve the right, in our sole and absolute discretion without liability to you or any third party, to terminate your use of the Bus Online Booking Service for any reason, including without limitation violation of this Terms of Service or other policies we may establish from time to time. / Tunahifadhi haki, kwa utashi wetu wenyewe bila kuwajibika kwako au kwa mtu mwingine yeyote, kusitisha matumizi yako ya huduma hii ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao kwa sababu yoyote ile, ikijumuisha bila kikomo ukiukwaji wa hivi Vigezo na Masharti au sera zingine zozote tutakazoiweka mara kwa mara.

No Endorsement of Bus Operators / Kuthibitisha Kampuni za Mabasi

Bus Online Booking Service does not represent or endorse any particular Bus Operator, and shall not be responsible for: (a) the safety, quality, accuracy, reliability, integrity or legality of any Bus Operating Company, the truth or accuracy of the description of the bus service put forward by the Bus Operator, or of any advice, opinion, offer, proposal, statement, data or other information (collectively, “Content”) displayed or distributed, purchased or paid through the Bus Online Booking Service; or (b) the ability of Buyers to buy Travel Service or Sellers to deliver Travel Services. Bus Online Booking Service hereby disclaims any liability or responsibility for errors or omissions in any Content or in the Service. / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao haiwakilishi wala kuthibitisha kampuni yoyote ya mabasi, na kwa hiyo haitawajibika kwa: (a) usalama, ubora, usahihi, uhakika au uhalali kisheria wa kampuni yoyote ya mabasi, ukweli au usahihi wa maelezo ya huduma ya usafiri yaliyotolewa na kampuni ya mabasi, au ushauri, maoni, mapendekezo, matamko, taarifa zozote (kwa ujumla, "maudhui") yaliyoonyeshwa, kutangazwa au kusambazwa, yaliyonunuliwa au kulipiwa kupitia huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao; au (b) uwezo wa Wanunuzi kununua huduma za usafiri au Wauzaji kutoa huduma za usafiri. Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao inajivua kuhusika na madhara yoyote au kuwajibika kutokana na kukosewa au kutoonyeshwa kwa jambo lolote katika maudhui au katika huduma.  

Limitations of Liability; Force Majeure / Kikomo cha Madhara; Force Majeure

Bus Online Booking Service shall not be liable to the Buyer in the event of any disruption of the Service or the Online Payment Platform or any part thereof resulting from Force Majeure and Bus Online Booking Service may suspend the Service or part thereof in such an event. Force Majeure for purposes of this Terms of Service means any situation or event that makes it impossible for Bus Online Booking Service to perform its obligations and includes but is not limited to any act of God such as lightning, floods, earthquakes, prohibitive decisions made by the government or local authority or civil war conflict and industrial strikes as well as any global or partial dysfunction of the Service caused by disruption or suspension of the telecommunication facilities. / Huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao haitawajibika kwa Mnunuzi kama itatokea huduma kukatizwa kwa kutofanya kazi kwa mfumo wa booking au wa malipo kwa mtandao kulikosababishwa na Force Majeure na huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao inaweza kusitisha huduma yote au sehemu ya huduma ikitokea hivyo. Force Majeure kwa vigezo na masharti haya inamaanisha hali yoyote au tukio linalofanya huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao isiweze kutimiza majukumu yake na inajumuisha pamoja na mambo mengine matukio ya nguvu za Mungu kama radi, mafuriko, tetemeko, maamuzi ya serikali kuu au serikali za mitaa, vita, ugomvi, migomo, maandamano pamoja na kutofanya kazi kwa sehemu au mfumo mzima kunakotokana na kuharibika au kutofanya kazi kwa mfumo wa mawasiliano. 

Jurisdiction; Governing Law / Wigo wa Sheria; Sheria Itakayotumika

This Terms of Service shall be governed in all aspects in accordance with the Laws of Tanzania and a court of competent jurisdiction in Tanzania shall determine every claim or dispute arising out of or in connection with this Terms and Conditions of Service. / Vigezo na Masharti haya yatatawaliwa katika nyanja zote kwa mujibu wa Sheria za Tanzania and mahakama za Tanzania ndizo zitakazotumika kuamua madai na kusuluhisha mizozo itakayotokana au kuhusiana na hivi Vigezo na Masharti.

Modification of Terms of Service for Buyers / Marekebisho ya Vigezo vya Huduma kwa Wanunuzi

We reserve the right, in our sole and absolute discretion, to change, modify, or amend any portion of this Terms of Service at any time by posting notification on Bus Online Booking website or otherwise communicating the notification to you. The changes will become effective, and shall be deemed accepted by you, after the initial posting and shall apply on a going-forward basis with respect to bookings initiated after the posting date. In the event that you do not agree with any such modification, your sole and exclusive remedy is to terminate your use of the Service. / Tunahifadhi haki, kwa uamuzi na utashi wetu wenyewe, kubadili, kurekebisha, au kukarabati sehemu yoyote ya Vigezo na Masharti haya wakati wowote kwa kutoa tangazo katika tovuti ya huduma ya kufanya booking za mabasi kwa mtandao au kwa kuwasiliana na wewe moja kwa moja. Mabadiliko yataanza kufanya kazi na yatachukuliwa kuwa umeyakubali baada ya kutumwa na yatatumika kuanzia wakati yalipotumwa kwenda mbele kwa maana ya bookings zitakazofanyika baada ya siku ilipotumwa hiyo taarifa. Endapo kama hukubaliani na marekebisho hayo, njia pekee uliyo nayo na kusimamisha na kuacha kutumia huduma hii.

© Copyright 2017 Kicheko Ltd, All rights reserved